Kenya Top Stories

Categories
Uncategorized

KOMESHENI WIZI WA MIFUGO ASEMA MBUNGE WA TURKANA YA KATI JOSEPH EMATHE

by Jeff Kizzilah

Ukosefu wa usalama na wizi wa mifugo katika eneo la Turkana umechangia pakubwa kusalia nyuma kimaendeleo katika maeneo hayo uku watoto na jamii izo zikisalia na makovu mengi kutokana na kuporwa kwa mifugo wao na kuuwawa kwa watoto na kina mama wakati wa mashambulizi ya wizi wa mifugo,hii imekua donda sugu na kitendawili ambacho serikali imeshindwa kutegua kwa muda wa zaidi ya miongo miwili uku jamii husika zikishiriki mashambulizi ya kulipiza kisasi ambayo kwa mwezi huu wa January pekee yamepelekea jumla ya takriban wakazi kumi na tano kuuwawa kwa mujibu wa mbunge wa eneo hilo.

Wakiongea mjini Mombasa wakati wa kongamano la wabunge katika hoteli Moja,mbunge wa Turkana ya kati na mwenzake wanaopakana wa eneo bunge la Loima Jeremiah Lomurukai wamesema kwamba ni sharti serikali ilinde maisha na Mali ya wakenya wote na kuhakikisha imekomesha mashambulizi ya mara kwa mara kwa kuongeza askari wa akiba wenye mafunzo ya juu ili kukabiliana na wahuni hao ambao kwa mda mrefu wameangaisha maeneo hayo.

Aidha wabunge hao wameilaumu jamii ya nchi jirani Uganda almaarufu karamojong kwa kushiriki uporaji mifugo na mashambulizi ya kulipiza kisasi ambayo yanauwa watoto na akina mama wasio kua na hatia.

Licha ya serikali kusema kwamba itakomesha milio ya risasi katika maeneo hayo
Hakuna hatua zozote zilizopigwa ili kuregesha amani maeneo hayo ivyo basi wananchi kubaki kuhangaika mikononi mwa wezi sugu wa mifugo uku viongozi wa eneo ilo wakikashfu vikali wanaoshiriki wizi wa mifugo ambao kulingana nao ni vigogo wa siasa na viongozi wenye ushawishi mkubwa serikali wakiongezwa na mbunge wa Tiaty William kamket ambayo mara kwa mara ametiwa nguvuni akihusishwa na wizi wa mifugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *